Wednesday, April 23, 2014

MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA KILOSA AWATAKA MADEREVA KUFUATA KANUNI NA TARATIBU ZA BARABARANI.



Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Masalu Mayaya amewataka madereva wanaoendesha vyombo vya moto kufuata kanuni na taratibu ya barabara.

Ameyasema haya wakati akizungumza na HABARIKWANZA  kuhusu  ujenzi wa uzio wa Shule ya  Msingi  Mazinyungu ambao unagharimu kiasi cha shilingi milioni miamoja arobaini na saba miambili themanini na tano na mia nane thelathini elfu na kusema  kuwa ujenzi huo kwa sasa upo kwenye utaratibu na kusema kuwa bado hakuna fungu la fedha kwa ajili ya ujenzi huo kwa sasa na kuwaomba wadau kujitokeza kwa ajili ya kuweza kufanikisha shughuli za ujenzi huo.

Pia Mayaya amesema kuwa kutafanyika utaratibu kwa ajili ya kuweka matuta katika eneo hilo la shule ya msingi mazinyungu ili kuzuia kutokea kwa ajali eneo hilo, pia ameongeza kwa kusema kuwa madereva waendelee kupewa elimu kuhusu matumizi ya barabara.

Naye Mkuu wa Shule hiyo  ya Msingi Mazinyungu Lameck Mkude amesema kuwa shule hiyo inakitengo maalumu cha watoto walemavu wapatao 74 wavulana 44 , wasichana 30 amesema kuwa wanahitaji uzio kwa ajili ya usalama wa watoto hao na mali zao. Pia Mkude amesema kuwa pindi ujenzi wa uzio huo utakapokamilika utafanya mali za shule na watoto hao kuwa salama kutokana na baadhi  ya watu wasiokuwa na nia njema na watoto hao. Na kuongeza kuwa kitengo hicho cha watoto walemavu kuna watoto wenye ulemavu wa ngozi (albino) ambapo kuna baadhi ya watu  kuwa na imani potofu.

No comments:

Post a Comment