Wednesday, April 2, 2014

WAKAZI WA KILOSA WAATHILIWA NA MAFURIKO KUTOKANA NA KUTOJALI MIUNDOMBINU YAO



Imeelezwa kuwa wakazi wa kata ya mbumi wilayani kilosa wanaadhiliwa na mafuriko ya mara kwa mara kutokana na mifereji kuwa michache na iliyopo kujaa tope pamoja na wananchi kutumia mifereji hiyo kutupa takataka ndani ya mifereji hiyo.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa kitongoji cha Mbumi B Ally Mdimu na kuongeza kwa kusema kuwa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani kilosa kumekuwa na chemchem ya maji mengi yanayoweza kusababisha athari katika makazi ya watu hivyo amewataka wananchi kuwa makini na matumizi  mazuri ya misingi inayotumika kusafirishia maji kwani amesema kuwa kuna baadhi ya wananchi wanatupa takataka katika misingi hiyo

Aidha mtendaji wa kata ya Mbumi Rajabu Mhina amewataka wananchi kuyajari mazingira yao kwa kuyafanyia usafi na kuacha tabia ya kuitegemea serikari  kwa kila kitu.

Nao wananchi wa kata hiyo ya Mbumi Sarehe Nasoro Hamisi na Paskolina Mtinda wanawaomba wananchi wenzao kuyajali mazingira yanayowazunguka na kuacha tabia ya kutupa takataka katika misingi hiyo inayopitisha maji hayo.

No comments:

Post a Comment