Thursday, April 10, 2014

WAKAZI WA KILOSA WAENDELEA KUTESWA NA MAFURIKO



Imeelezwa kwa zaidi ya kaya 208 za kitongoji cha Rozi kata ya magomeni wilyani kilosa hawana mahali pa kuishi  kutokana na mafuriko yaliyotokea  yametokana na mvua zinazoendelea kunyesha wilyani humo.
Hayo yameelezwa april 9 mwaka 2014 na mwenyekiti  wa kitongoji cha Rozi Bw Abdul Bona wakati akiongea na HABARI KWANZA  ofisini kwake na kusema kuwa anaiomba serikali kuwatengea eneo maalum wahanga hao wa mafuriko. Bw Bona amesema kuwa  wahanga hao kwa sasa wanishi kwa zao na wengine wanaishi katika nyumba ambazo zimebomolewa hivyo wanahitaji msaada.
                                               
                                    Kati ya Nyumba zilizoathilika katika Kitongoji hicho
Pia ameomba watendaji wa ngazi za juu kushirikiana na serikali za vijiji hasa katika majanga kama haya ameongeza kuwa katika mafuriko ya mwaka 2009/2010 serikali iliwaombia wahanga watawapatia sehemu ya kuishi jambo ambalo halijatekelezwa mpaka sasa.
                           
                                  
                                       Baadhi ya makazi ya watu wa Kilosa  yalivyoathiriwa na mafuriko yaho.
Amesema anaomba serikali kuwaangalia wahanga hao kwa jicho la tatu kwani mvua bado zinaendelea hivyo hawajui siku za usoni hali itakuwaje.
                                            Barabara zikiwa zimejaa maji

 Akiongea mmoja kati ya wahanga hao bi Zaituni Nassoro amesema licha ya mafuriko hayo kuharibu vitu vya nyumbani pia yameharibu mazao ya shambani kwa kiasi kikubwa hivyo kuwaacha na hofu kubwa ya kukubwa na baa la njaa.

No comments:

Post a Comment