Saturday, April 26, 2014

WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA MISITU WILAYANI KILOSA



Afisa Misitu wa Wilaya ya Kilosa Othman Haule ameitaka Serikali kuwekeza  katika sekta ya mali asili na misitu kwani ni sekta nyeti nchini.

Ameyesema hayo ofisini kwake wakati akizungumzia jinsi misitu inavyoathiliwa na wananchi kwa matumizi ya Kila siku na kusema kuwa chanzo cha misitu hiyo kuharibika ni kutokana na serikali kutoipa kipaumbele sekta hiyo ya maliasili na kusema kuwa changamoto  inayowakabili ni baadhi ya wananchi kutokujua umuhimu wa misitu na kuitumia vibaya kwa uchomaji mkaa hovyo kilimo ndani ya misitu , pamoja na ufugaji horela na kutolea  mfano  msitu wa mamiwa kisara North ulivyohalibiwa kwa shughuli za Kilimo pamoja na misitu ya Gairo ilivyoharibiwa kwa Ufugaji horela wa mifugo na uchomaji wa mkaa na kusababisha eneo hilo kuwa jangwa.

                                         misitu ya maguha wilayani gairo jinsi ilivyoathiliwa na ufugaji horela.

Pia amewaasa wananchi wanaokaa pembezoni mwa misitu kuacha kufanya shughuli za uhalibifu wa msitu ikiwemo uchomaji moto kwa ajili ya uwindaji shughuli za kilimo  pamoja na uchomaji wa mkaa. Na kuongeza kwa kusema kuwa anawataka wananchi kuitunza vizuri misitu ili kuweza kuendelea  kupata mvua kwa wingi na kuondokana na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyopo kwa sasa. 
 













Tanki la maji likiwa likiwalimekauka kutokana na ukame uliopo sehgemu hiyo uliotokana na ufugaji horela na uchomaji wa mkaa.
 Mashamba yakiwa katikati mwa msitu wa mamiwa kisara North kata ya lumbiji wilayani kilosa.
Aidha amesema kuwa kila mwananchi anajukumu la kutunza misitu kwa kusema kuwa mwananchi anapoona magunia ya mkaa barabarani akae akitambua kuwa kuna misitu imeteketea na kusisitiza kuwa kila mwananchi anapaswa kuwa mlinzi wa mwenzake.
  
 biashara ya mkaa maguha yazidi kuteketeza misitu wilayani gairo

No comments:

Post a Comment