Saturday, July 12, 2014

MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA SABA AFICHWA NDANI KUTOKANA NA KUWA NA ULEMAVU WILAYANI KILOSA



Mtoto anayefahamika kwa jina la Devota Dalule mwenye umri wa miaka saba (7)  mkazi wa Dumila Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro amefungiwa ndani  kwa muda wa miaka saba na Mama yake mzazi anayetambulika kwa jina la Sarah Mazengo mwenye umri wa miaka 39 mkazi wa Dumila Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro kutokana na mtoto huyo kuwa na ulemavu wa miguu .
                                         Mtoto Devota Dalule akiwa hopspitali ya wilaya ya kilosa

Kwa mujibu wa Daktari Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Kilosa Shedrack Mponzi amesema mtoto  huyo amefika hospitalini hapo  usiku wa kuamkia julai 12 mwaka huu akiwa  tatizo la Utapiamlo na kusema kuwa hali yake bado haijatengemaa na leo hii amepewa rufaa ya kwenda hospitali ya mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi.

                                  MtotoDevota Daluleakiwa hospitali ya wilaya kilosa akiendelea kupatiwa matibabu

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii wilayani Kilosa Saidi Kataluma amesema kuwa matatizo haya ya utesaji na unyanyasaji wa watoto kwa wilaya ya Kilosa tatizo hilo ni la pili la kwanza limetokea julai 3 mwaka huu lililomuhusisha mtoto aliyefahamika kwa jina la Selemani Salumu mwenye umri wa miaka mitatu (3) ambaye ametelekezwa na mama yake mzazi Mwamini Juma mwenye umri wa miaka 20 kutokana na mtoto huyo kuwa na kichwa kikubwa. Na tukio la pili ni hili la mtoto Devota Dalule ambapo inasemekana mtoto huyo amewekwa ndani kwa kipindi chote cha miaka saba na kutopata huduma muhimu kama chakula pamoja na mavazi na inasemekana kuwa mama huyo humficha mtoto huyo uvunguni ili asionekane kwa watu kutokana mtoto huyo kuwa na ulemavu.
                                     muuguzi wa hospitali ya wilaya kilosa akimuhudumia mtoto Devota Dalule


Kataluma amewataka wananchi kuendelea kufichuwa maovu yote yanayotendeka katika jamii kwa ajili ya kutokomeza matatizo hayo ya ukatili dhidi ya watoto wadogo.
Kwa upande wao wananchi wa Wilayani  Kilosa Lameck Mkude na Jane Amandus wamesema kuwa vitendo hivi vinahathiri sana ukuaji wa mtoto na wameviomba vyombo vya sheria pamoja na wananchi kusimamia mambo haya kwa ajili ya kuweza kuyatokomeza na wameongeza kuwa mtoto hata kama atakuwa na ulemavu ana haki ya kuishi kama mtoto asiye na ulemavu.

No comments:

Post a Comment