Shirika lisilokuwa la
kiserikali HUDESA linalofadhiliwa na USAID Kwa ushirikiano na AFRICARE
linaendesha mafunzo ya lishe bora kwa kina mama wajawazito na wanaonyonyesha kwa
lengo la kupunguza vifo vya kinamama wajawazito na watoto walio chini ya umri
wa miaka miwili wilayani kilosa mkoani morogoro.
Afisa mradi ustawi wa HUDESA wilayani kilosa Hawa Hatibu
Akizungumzia malengo ya
HUDESA julai 22 mwaka huu Afisa ustawi wa shirika hilo wilayani kilosa Hawa
Hatibu amefafanua kuwa mwanzo bora ni siku elfu moja akiwa na maana toka motto
yupo tumboni hadi kuzaliwa kwake na kufikia umri wa miaka miwili [2]ameeleza
kuwa kitaalamu motto anapokosa lishe bora kwa kipindi hicho anaweza kudumaa
kiakili na kimwili.
Bustani ya kiroba
Aidha ameongeza kwa kusema
kuwa katika mpango huo wa mwanzo bora wanafundisha kinamama jinsi ya kuandaa
chakula bora kwa mtoto sambamba na hapo wameandaa bustani ya mbogamboga za
majani pamoja na viazi lishe ambavyo hutumika kumuandalia chakula mtoto.
Baadhi ya walezi wakiwa kwenye bustani
Kwa upande wake Salehe
kaombwe ambaye na mhudumu wa afya wa majumbani kata ya kasiki wilayani kilosa
amesema kuwa wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kuepukana na vifo vya
kinamama na udumavu wa watoto.
Bustani ya mbogamboga aina ya chainizi
Nao baadhi ya kinamama wa
wilayani kilosa mkoani morogoro Husna Rashidi na Amina bint Ally wamesema kuwa wanalishukuru
sana shirika la HUDESA kwa kuwapatia elimu ya mafunzo ya jinsi ya kuwaandalia
lishe iliyobora watoto wao ili waweze kukua vizuri na kuweza kuepukana na
magonjwa yanayoepukika.
No comments:
Post a Comment