Thursday, June 12, 2014

AFARIKI DUNIA AKIWA LINDONI WILAYANI KILOSA



Mkazi wa mjini wilayani kilosa aliyetambulika kwa jina la Abdallah Ramadhani aliyekadiliwa kuwa na umri wa miaka 60 ambaye alikuwa mlizi wa ofisi za chama cha mapinduzi ( CCM) wilayani Kilosa amekutwa amefariki usiku wakuamkia juni 12 mwaka huu
Akizungumzia kifo hicho motto wa marehemu Ramadhani Abdallah amesema kuwa baba yake alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa shindikizo la damu na alipatiwa matibabu juni 9 mwaka huu na kuambiwa arudi juni 12 kwa matibabu zaidi, na ameongeza kwa kusema kuwa marehemu baba yake ameacha watoto tisa na wake watatu.
Akifafanua tukio hilo katibu wa chama cha mapinduzi Wilayani Kilosa Dodo Sambu amesema kuwa mlinzi huyo ni kweli alikuwa akifanya kazi katika ofisi hiyo ila hawakuwa na taarifa yoyote ya ugonjwa ya mlinzi huyo.
Kwa upande wake mhudumu wa ofisi hiyo ya CCM wilaya ya kilosa Hamisi Ally ambaye yeye analala ofisi hapo ameeleza kuwa yeye alipoamka asubuhi alikuta mwili wa mlinzi huyo ukiwa umelala chini na kueleza kuwa katika ulalaji aliomkuta alihisi kuwa amefariki.
Akithibitisha tikio la kifo hicho hicho kaimu mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya kilosa masale Dickson ameeleza chanzo cha kifo hicho kuwa ni tatizo la shindikizo la damu lililokuwa juu sana na ndio lililompelekea kifo chake.

No comments:

Post a Comment