Wednesday, June 11, 2014

KIASI CHA SHILINGI MILIONI 30 ZA TARAJIWA KUTUMIKA KATIKA KUUPOKEA MWENGE WA UHURU WILAYANI KILOSA.



Serikali wilayani Kilosa imetaja miradi itakayo zinduliwa na mbio za mwenge mwaka huu ndani ya wilaya ya Kilosa.
Akizungumzia miradi hiyo juni 11 mwaka huu Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Elias Tarimo mnamo june 23 mwaka huu mwenge utapokelewa ukitokea wilaya ya kilombero na kukiombizwa wilayani kilosa , Ukiwa ndani ya wilaya ya Kilosa mwenge huo utazindua miradi saba ambayo ni pamoja na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa maji mikumi uliyogharimu jumla ya shilingi milioni mia nane , kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa kukoboa ya vijana ilakala, kuweka jiwe la msingi katika  hosteli ya shule sekondari  isanga , ufunguzi wa kituo cha kupima VVU ulaya  .
Amesema miradi hiyo amabayo imegharimu fedha nyingi ni lazima wananchi waakikishe inaendelezwa na si kufia njiani kama inavyojitokeza katika baadhi ya miradi inayoanzishwa , kwani hayuko tayari kuona miradi ikiteketea na kuona fedha za wananchi zikipotea bila kuleta faida .
Mwenge huo utakimbizwa ndani ya wilaya ya Kilosa kwa siku moja na utalala kata ya kisanga kabla ya kukabidhiwa kwenye uongozi wa mkoa ambapo ndipo   utakapo kuwa mwisho wa mbio za mwenge katika wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro baada ya hapo uongozi wa mkoa utaukabidhi mwenge huo mkoani Iringa .
Pia ametoa wito kwa wanaqnchi wa kilosa kutoa michango ili kufanikisha mbio hizo kwani hadi kukamilisha mbio hizo zinahitajika milioni 30 na kusema kuwa  hadi sasa wamekusanya kiasi cha shilingi milioni 15.

No comments:

Post a Comment