Wednesday, June 25, 2014

KESI YA MSICHANA ALIYEBAKWA NA WANAUME 6 NCHINI KENYA YAZUA MAANDAMANO





Kesi dhidi ya mshukiwa mmoja anyetuhumiwa kumbaka msichana mmoja katika eneo la Bumala Magharibi mwa Kenya imeahirishwa. 

Mshukiwa mmoja kati ya sita wanaodaiwa kumbaka na kumtupa katika shimo msichana huyo kwa jina Liz, alifikishwa kizimbani na kufunguliwa mashtaka ya kumbaka na kujaribu kumuua msichana huyo, katika kisa ambacho kimezua hasira na hamasa miongoni mwa wakenya wa tabaka zote

Kinyume na kesi zingine, kesi hii iliendeshwa faraghani huku mawakili wanaowakilisha pande husika na maafisa wa mahakama ndio walioruhusiwa kuwepo mahakamani.

Afisa kutoka ofisi ya mwendesha mashitaka mkuu aliwaambia waandishi wa habari kuwa ni mkubwa pekee ambaye anapaswa kuzungumzia suala hili, kutokana na uzito wake.

Mawakili wa mshichana huyo wamesema kuwa wao waliamua kuomba kesi hiyo kuendeshwa faraghani ili kumlinda mhusika ambaye yuko chini ya umri wa miaka 18. Pia uamuzi huo ulichukuliwa ili kuwapa wanaohusika Imani ya kutoogopa mtu yeyote.

Mwandishi wa BBC ambaye yuko mjini Busia Robert Kiptoo, anasema kuwa kinyume na ilivyokuwa Jumatatu wakati mamia ya watu waliandamana, leo hali ilikuwa shwari huku jamaa na marafiki tu ndio waliofika mahakamani.

Liz alitoa ushahidi wake leo asubuhi na kisha kuhojiwa nyakati za alasiri kuhusiana na tukio hilo ambalo lilimuacha kama amelemazwa kabisa.

Washukiwa wengine watano bado wanasakwa na polisi na duru zinasema kuwa wazazi wao wamepewa ilaani kuwawasilisha washukiwa hao mahakamani.

Liz inadaiwa alibakwa na wavulana sita Juni mwaka jana na kututwa katika shimo la choo, hali iliyosababishia majeraha ambayo kwa sasa yamemlemaza.

Tangu wakati huo wanaharakati wa kijamii wamekuwa wakishinikiza mkuu wa polisi nchini Kenya kuhakikisha kuwa waliombaka Liz wamefikishwa mahakamani.

Hata hivyho sakata hiyo ilichukua mkondo tofauti pale, ilipofichuliwa kuwa waliombaka waliachiliwa huru na polisi baada ya kuadhibiwa kufyeka nyasi katika kituo kimoja cha polisi.

Kesi dhidi ya mshukiwa mmoja wa ubakaji wa msichana Liz na kumjeruhi vibaya nchini Kenya imeahirishwa hadi tarehe 8 mwezi Juni. 

Kesi ya Liz ilisababisha ghadhabu sana sio Kenya tu bali duniani kote hasa kwa ambavyo polisi waliishughulikia.
Muungano wa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayopinga dhuluma dhidi ya wanawake, uliongoza waandamanaji ambao baadaye walikusanyika katika kituo cha mkuu wa jimbo, Isaiah Nakoru.
Liz alibakwa mwaka jana na kuachwa na majeraha mabaya mwilini mwake
Walimkabidhi mkuu huyo nyaraka zilizotiwa saini kutaka Liz atendewe haki.

Waliotia saini nyaraka hizo wanamtaka mkuu wa polisi kuwakamata washukiwa na kitendo hicho cha unyama dhidi ya Liz ambao walimbaka na kisha kutupa mwili wake ndani ya shimo lenye urefu wa futi 25 mjini humo.

Viongozi wa maandamano wanasema kuwa idadi kubwa ya wasichana waliobakwa tangu kusikika kwa kisa cha Liz wamekuwa wakienda kuwashitaki watuhumiwa kwa polisi.
Liz alibakwa na wanaume sita ambao walimuwacha na majeraha mabaya kwenye mwili wake kiasi cha kulazwa hospitalini kwa miezi kadhaa.

Mamake Liz alikuwa miongoni mwa waandamanaji.

No comments:

Post a Comment