Tuesday, June 10, 2014

WATOTO MAPACHA WAFA MAJI PWANI



Watoto mapacha wenye umri wa miaka sita wamekufa baada ya kutumbukia kwenye kisima cha maji wakati wakicheza.
Kamanda wa polisi mkoa wa pwani Ulrchi Matei amesema watoto hao wametumbukia kwenye kisima kilichojirani na nyumbani kwao ambapo baada ya pacha wa kwanza kuona mwenzake anazama alikwenda na kutaka kumuokoa ndipo naye alipozama.
Kwa mujibu wa kamanda huyo tukio hilo la june 8 mwaka huu majira ya saa kumi jioni katika kijiji cha pipani kiwangwa kata ya kiwangwa tarafa ya msata wilaya ya bagamoyo.
Ameeleza kuwa miili ya watoto hao mapacha baada ya kuopolewa ilikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya maziko .

No comments:

Post a Comment