Friday, June 27, 2014

WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA WATAKIWA KUJADILI NA KUCHAMBUA RASIMU YA PILI YA KATIBA ILI KUPATA KATIBA ILIYO BORA KWA KILA MWANANCHI WA KITANZANIA



Wito umetolewa kwa wote wanaohusika katika mchakato wa kupata katiba mpya kungalia maslahi ya Taifa kwanza badala ya kuangalia maslahi binafsi au ya vyama vyao.
Hayo yamesemwa na afisa wa shirika la Oxfam nafasi za wanawake katika kupata Katiba Mpya Heri Ayubu wakati wa mdahalo wa mchakato wa katiba na jinsia uliofanyika Juni 26 na kuwahusisha Wanawake mbalimbali kutoka tarafa ya Kilosa.
Ayubu amesema tangu kuanza kwa mchakato wa kupata katiba Mpya kumekuwepo na changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya makundi kuvutia kwake hususani watu wa vyama vya siasa hali inayotoa mashaka ya kupatikana kwa katiba nzuri iliyopendekezwa na wananchi.
Aidha ayubu ameongeza kusema kuwa wanaendelea kutoa elimu mbalimbali kwa wadau hususani wanawake ili muda utakapofika wakati wa kupiga kura ya  katiba wawe na ufahamu mkubwa ju ya katiba hiyo  maamuzi watakayotoa yawe sahihi.
Kwa upande wa wajumbe waliohudhulia mdahalo huo mwalimu Sikuzani Mfinanga  na Rehema Mhini kwa niaba ya wanawake wenzao wamesema kuwa wanashukuru kwa kufanyika kwa mdahalo kwani umeweza kuwapanua kifikra na wamewaomba wajumbe wa bunge maalumu la katiba kuheshimu mawazo yao na kutoa wito kwa wanawake nchi kuisoma kwa makini katiba mpya itakapotoka na kujitokeza katika kuipigia kura.
Mdahalo huo umeandaliwa na shirika la msaada wa kisheria morogoro Palaregal kwa kushirikiana na mashirika ya Restress Development,

No comments:

Post a Comment