Wednesday, June 18, 2014

CHAMA CHA CUF CHASHINDWA KUFANYA UCHAGUZI WA VIONGOZI WILAYANI KILOSA



Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha Wananchi( CUF) Wilayani  Kilosa Mkoani Morogoro uliokuwa ufanyike juni 15 mwaka huu umehairishwa kutokana na sababu mbalimbali hadi utakapotajwa tena na Uongozi wa Wilaya.

Hali hiyo imejidhihirisha katika Ukumbi wa Manyovu uliopo Wilayani Kilosa ambapo ndipo Uchaguzi ulipangwa kufanyika saa mbili usiku  ili kuweza kuchagua Viongozi mbalimbali wa Wilaya mara baada ya kushindwa kuhudhuria robo tatu ya wajumbe wa Chama hicho.
Kwa mujibu  wa Mjumbe wa Uchaguzi ngazi ya Taifa Husein Shaban Mwakikoti amesema kuwa mkutano huo ulikusudiwa kuwa na wajumbe mia tatu lakini hadi kufikia saa tano usiku wajumbe mia moja na ishirini tu ndio waliokuwa wamewasili,hali iliyosababisha kuahirishwa kwa uchaguzi  kwa mujibu  wa Katiba ya chama hicho inayosema kuwa Uchaguzi utafanyika kama kutakuwa na  nusu ya wajumbe wote.
Ameongeza kwa kusema kuwa sababu kubwa iliyosababisha wajumbe kutohudhuria Mkutano wa Uchaguzi ni pamoja na ucheleweshwaji wa Taarifa kwa wajumbe pamoja na  umbali  kulingana na jiografia ya wilaya ya Kilosa kwani wajumbe wengine hawakufika kabisa .
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria Mkutano huo wamemuomba Msimamizi Mkuu wa uchaguzi  Husein Mwakikoti kupeleka kwenye uongozi wa Taifa changamoto mbalimbali zilizoko ndani ya Wilaya ya Kilosa ikiwemo Ruzuku ndogo ambayo haikidhi mahitaji ukilinganisha na ukubwa wa Wilaya.

No comments:

Post a Comment