Friday, June 6, 2014

BRN YAZIDI KUPAMBA MOTO WILAYANI KILOSA

Katika kukuza kiwango cha ufaulu na kutekeleza mpango wa matokeo makubwa sasa [BRN]shule ya msingi mazinyungu imetoa zawadi kwa wanafunzi waloshika nafasi ya kwanza hadi ya tatu katika mhula huu wa kwanza ambapo June 6, 2014 mmwaka huu shule za msingi zimefunga kwa likizo ya muda wa mwezi mmoja.
Katika utoaji wa zawadi hizo mwalimu mkuu wa shule hiyo Lameck mkude amesema kuwa wametoa zawadi hizo kwa wanafunzi walioshika nafasi hizo kwa ajili ya kuleta mwamko wa kukazana kusoma kwa bidii kwa wale ambao hawakufanya vizuri kwa mhula huu wa kwanza.
Pia amesema kuwa tatizo la kushuka kwa kiwango cha ufaulu shuleni hapo ni pamoja na utoro wa rejareja na baadhi ya wazazi kuwapa wanafunzi kazi za kibiashara muda wa masomo na baada ya masomo na amewataka wazazi kuachana na dhana hiyo ya kuwafanyisha kazi watoto na badala yake wawatengee muda wa kujisomea.
Aidha mwalimu wa taaluma wa shuleni hapo Isaya mlimi amesema kuwa katika kukuza kiwango cha ufaulu shuleni hapo wameibua mbinu ya kuwataja wale wanafunzi kumi dhaif walioshika nafasi ya chini na wale wanafunzi bora walioshika nafasi ya juu lengo likiwa ni kuwahamasisha wale ambao hawakupata alama nzuri za ufaulu.
Kwa upande wao wanafunzi waliopata alama za chini yaani wale kumi dhaifu wamesema kuwa sababu iliyowapelekea wao kutokufaulu ni kutopata muda wa kujisomea kwa kupewa kazi za nyumbani na wanapomaliza huwa wanakuwa wamechoka na kushundwa kujisomea.
Aidha kwa upande wa wanafunzi waliofaulu kwa wastani mzuri Abdalah chandafa,kwini Zuberi na Hasani Isumaili wamesema kuwa wao wamefaulu vizuri kwa sababu walikuwa wanawasikiliza walimu kwa umakini na kuongeza kuwa nidhamu nayo imewafanya kufanya vizuri katika mitihani yao.

No comments:

Post a Comment