Thursday, June 19, 2014

ALIYEKUWA DIWANI WA KATA YA MKWATANI WILAYANI KILOSA AFARIKI DUNIA

Aliyekuwa diwani wa kata ya mkwatani kupitia chama cha mapinduzi CCM Amina mwarabu amefariki usiku wa kuamkia june 19 mwaka huu.
Akuzungumzia kifo hicho mtoto wa marehemu Ally Nassoro amesema kuwa mama yake alikuwa na maradhi ya moyo na kisukari ambayo yalikuwa yakimsumbua kwa muda mrefu na ndiyo yanayosadikika kupelekea kifo chake.Na amefafanua kuwa marehemu mama yake amefariki akiwa na umri wa miaka 62 na ameacha jumla ya watoto wane [4]wanaume watatu na wakike ni mmojana wote hao wanajitegemea.
Akiongea kwa niaba ya chama cha mapinduzi [CCM] wilayani kilosa katibu msaidizi wa chama cha mapinduzi Twaribu Kassim Kaberege amesema kuwa wameupokea msiba huo kwa masikitiko makubwa kwani marehemu alikuwa mwenyekiti msaidizi katika baraza la wazee wilayani kilosa pia alikuwa mwenyekiti wa vijana wilaya ya kilosa na amesema kuwa limekuwa pengo kubwa kwa jamii ya kilosa na taifa kiujumla kwani marehemu alikuwa ni mpiganaji wa maendeleo.

No comments:

Post a Comment