Tuesday, June 10, 2014

MKUU WA WILAYA YA KILOSA AWATAKA WAKUU WA IDARA KUKUSANYA MICHANGO YA MWENGE




Imeelezwa kuwa zaidi ya shilingi milioni kumi na sita zimekusanywa katika maandalizi ya kuupokea mwenge wa uhuru wilayani kilosa mkoani morogoro kutoka sehemu mbalimbali wilayani humo.
Hayo ameelezwa na mwenyekiti wa kikao hicho cha kamati ya sherehe za mwenge Elias Tarimo ambaye ni mkuu wa wilaya ya kilosa kilichofanyika wilani kilosa kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashuri mwishoni mwa wiki iliyopita.
Aidha Tarimo amewataka wakuu wa idara na watendaji wa kata kuwahimiza waliochini yao kuchanga michango hiyo ili kufanikisha sherehe hizo za mbio za mwenge.
Amesema mwenge wa uhuru unatarajiwa kupokelewa june 23 mwaka huu ukitokea kilombero ukiwa umebeba ujumbe usemao” Katiba ni sheria kuu ya nchi “wenye kauli mbiu isemayo JITOKEZE KUPIGA KURA YA MAONI ILI TUPATE KATIBA MPYA ambapo utazindua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mkuu wa wilaya ameongeza kusema kuwa miradi itayofunguliwa na mwenge ni pamoja na Hostel ya sekondari ya Kisanga kituo cha uhamasishaji wa kupima ukimwi ulaya na kuweka jiwe la msingi kwa kituo cha wakulima Isanga.

No comments:

Post a Comment