Saturday, June 14, 2014

MKUU WA WILAYA YA KILOSA AWATAKA WAZAZI KUACHA TABIA YA KUWATUMIKISHA WATOTO SHUGHULI ZA KIBIASHARA



Imeelezwa kuwa jamii ya kilosa inaongoza katika kuwatumikisha watoto wadodo katika shughuli za kibiashara.

Akizungumzia utumikishwaji huo wa watoto june 13 mkuu wa wilaya ya kilosa Elias Tarimo ametoa tamko kwa wazazi wote watakao bainika kumtumikisha motto shughuli za kibiashara atachukuliwa hatua kali za kisheria na kuwataka viongozi vijiji,kata na Tarafa kusimamia katika kusimamia katika kupatikana kwa haki za mtoto.

Naye Afisa ustawi wa jamii wilaya ya kilosa Saidi kataluma amesema kuwa wilaya ya kilosa inaongoza kwa utumikishwaji wa watoto walio chini ya umri wa miaka 18 na kueleza kuwa katika wilaya ya kilosa maeneo yanayoongoza kuwatumikisha watoto katika shughuli za kibiashara ni Mtendeni na Behewa na kuongeza kwa kusema kuwa wanajitahidi kutoa elimu  kwa jamii kutambua haki za mtoto na kuzifuata.

Kwa upande wa mwenyekiti wa kitongoji cha behewa Zainobi Eusobio amesema watoto wengi wanatumikishwa shughuli za kibiashara ni kutokana na hali ngumu ya kimaisha na kuwataka wananchi kuwa na ushirikiano katika kutetea haki za watoto.

Kwa upande wake fikira mtolera mkazi wa behewa ambaye ni baadhi ya wazazi wanaowapa kazi za kibiashara watoto amesema kuwa wanafanya hivyo kutokana na hali ngumu ya kimaisha na kupelekea kuwafanyisha kazi watoto hao na ameongeza kuwa serikali nayo haiwajali kwani  mara nyingi hupita kuwaandikisha majira katika familia zinazoishi katika mazingira magumu na hatimaye kutowapatia muafaka wa kuwaandikisha majina hayo.

No comments:

Post a Comment