Thursday, June 19, 2014

SOKO LA SABASABA WILAYANI KILOSA LA BOMOLEWA.

Wafanyabiashara wa soko la sabasaba lililopo wilayani Kilosa Mkoani morogoro wamelilalamikia uongozi wa CCM wilaya kwa kuwabomolea mabanda yao wanayofanyia biashara .
Wakizungumza hali hiyo ya uvunjaji wa mabanda ya sokoni hapo Baadhi ya wafanyabiashara hao Juma Maliwa na Mrisgo Samatta wamesema kuwa mabanda yao yamebomolewa hivi karibuni  sababu ikiwa ni kupisha ujenzi wa Flame za kibiashara ambapo wamedai kuwa flame hizo ambazo zitajengwa ni kwa ajili ya watu binafsi . Na wamelalamika kuwa katika ubomoaji huo wafanyabiashara hawakupewa muda wa kujiandaa kwa ajili ya kuhamisha bidhaa zao pia hawakuandaliwa mazingira ya kuhamishia biashara zao hali iliyopelekea wateja kupata usumbufu.
Naye katibu msaidizi wa soko hilo la sabasaba Juma Kigoma amesema kuwa mpango huo wa bomobomo ulikuwepo kwenye mpango na Lengo ni kuboresha hali ya soko hilo na kuongeza kuwa wafanyabiashara hao walipewa muda na miezi sita kwa ajili ya kujiandaa.
Kwa upande wake katibu wa chama cha mapinduzi wilayani Kilosa Twribu Kassimu Kaberege amesema kuwa bomobomo hiyo ni kwa vipande ambavyo havina watu lengo likuwa ni kuboresha soko hilo na kufanya wale ambao hawana nafasi ya kufanya biashara waweze kupata nafasi hiyo katika soko hilo.
Aidha ametoa ametoa wote kwa wito kwa wafanyabiashara wa soko la sabasaba wasifanyie biashara zao katika vibanda ambavyo  vimeezekwa kwa makuti na badala yake wametakiwa kuezeka vibanda vyao kwa bati.
Na ameongeza kuwa hawajatoa tanko la kuvunjwa kwa mabanda hayo ila waliwataka wafanyabiashara hao waviezeke vibanda vya kwa makuti.


No comments:

Post a Comment